AZAM VS YANGA DAKIKA 90 ZA MCHEZO ULIOFANYIKA LEO JUMAMOSI 5/3/2016 DAR ES SALAAM
Mchezo wa marudiano wa raundi ya pili wa ligi kuu kati ya Azam FC
ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huo umemalizika kwa timu hizo
kutoka sare ya kufungana magoli 2-2 mchezo ambao umechezwakwenye uwanja
wa taifa jijini Dar es Salaam.
Azam walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 12 ambalo lilitokana na
kujifunga mlinzi wa Yanga Juma Abdul baada ya Kipre Tchetche kupiga
shuti ambalo lilipanguliwa na golikipa wa Yanga Ally Mustafa ‘Barthez’
kisha Juma Abdul akajifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa.
Juma Abdul akaisawazishia Yanga bao hilo dakika ya 28 kwa shuti kali
ambalo lilijaa moja kwa moja wavuni likimshinda golikipa wa Azam Aishi
Manula.
Yanga wakapata bao la pili mfungaji akiwa ni Donald Ngoma aliyepasia
nyavu dakika ya 42 kabla ya John Bocco kusawazisha na kuufanya mchezo
huo kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
TAZAMA GOLI LA PILI LA YANGA HAPA.....
Category: