TED CRUZ AJITOA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS NCHINI MAREKANI
Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican amejitoa katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa kugombea urais ,alitoa tangazo la kujitoa mara tuu baada ya kushindwa kwa kura katika jimbo la Indiana.
Hata hivyo Ted Cruz ambae anafahamika zaidi kwa cheo chake cha Useneta katika jimbo la Texas aliomba radhi wafuasi wake na kuwaeleza namna alivyofanya jitihada za nguvu lakini anasikitika kuwa jitihada zake ziligonga ukuta kitu kilichompelekea yeye kushindwa kuona fursa ya yeye kuweza kusonga mbele zaidi katika mtanange huo.
Wafuasi wengi wa Crunz wamesikitishwa na kukatishwa tamaa na maamuzi hayo kitu kinachopelekea kumpa mpizani wake anaegombea kwa tiketi ya chama cha Republican MhTrump kuweza kupata nafasi kubwa ya kuweza kuchaguliwa katika uchaguzi huo.
Category:
0 comments