Maalum: Je wewe hukumbwa na maumivu ya mgongo?
Watu wenye maumivu ya mgongo wana uwezekano mkubwa wa maumbile ya mgongo wao kuwa sawa na ule wa sokwe.
Jeraha linalojitokeza katikati ya vipande vya mifupa ya uti wa mgongo ndio sababu tofauti ya maumbile.Jeraha hilo hubadilisha uti wa mgongo kwa kuwa binaadamu walibadiliko kutoka kutumia miguu minne hadi miguu miwili.
Watafiti wanasema kuwa matokeo yao yanaweza saidia madaktari kuwajua wale wanaokabiliwa na hatari ya kupata matitizo ya mgongo.
Utafiti huo uliochapishwa katika BMC revolution biology, uliwashirikisha wanasayansi kutoka Scotland, Canada na Iceland.
Timu ya utafiti ilichambua wanyama walio na uti wa mgongo kama vile sokwe, pamoja na mifupa ya kale ya binadamu ili kuchunguza uhusiano kati ya maumbile ya mifupa ya mgongo, harakati na afya ya mgongo wa binadamu.
Category:
0 comments