HATMA YA WANAJESHI WA BURUNDI SOMALIA HII HAPA
Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amesema ikiwa hatua ya kuondoa majeshi ya Burundi itafanyika nchini Somalia itaathiri mapambano dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.
Mwanzoni mwa juma hili Marekani ilitangaza kupunguza kiasi cha pesa inachotoa kwa majeshi ya Burundi baada ya shutuma kuwa jeshi hilo limejihusisha katika vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu wakati wakizima vurugu zilizojitokeza katika jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza liliposhindwa.Umoja wa mataifa ya Afrika AU, nayo imesita kupeleka kundi jingine la wanajeshi wa Burundi nchini Somalia.
Lakini Kay, amesema kuwa majeshi ya Umoja wa Afrika yanahitaji msaada kuweza kupambana na Al Shabaab.
Aidha Kay ametahadharisha kuongezeka kwa mahitaji ya kibinaadamu nchini Somalia na kutoa wito wa jumuia ya kimataifa kuendelea kupeleka misaada nchini humo.
Category:
0 comments