Wanasayansi watengeneza mbegu zakiume
Seli za mbegu za kiume zimetengezwa katika maabara kwa mara ya kwanza na hivyobasi kuwapa matumaini wanaume wasio na uwezo wa kupata watoto.
Kampuni moja nchini Ufaransa imedai kwamba imefanikiwa kubadilisha vipande tofauti vya maumbile hadi kupata mbegu za kiume zinazoweza kutoa mtoto kwa mara ya kwanza.
Iwapo uzinduzi huo utathibitishwa ,huenda ukabadilisha maisha ya wanaume wengi duniani ambao hawawezi kutoa mbegu za kiume.
Maabara ya Kallistem,kituo cha kibinafsi cha utafiti kilichopo mjini Lyon kimesema kuwa kitaweza kufanya majaribio katika kipindi cha miaka miwili.
Iwapo uzinduzi huo utaingia sokoni,kampuni hiyo inataraji kuwatibu watu 50,000 kila mwaka soko ambalo linaweza kuwa na thamani ya pauni bilioni 1.7 .
Hatahivyo matokeo ya utafiti huo hayajachapishwa ama hata kuthibitishwa huku wataalam wa Uingereza wakichukulia uvumbuzi huo kama uvumi tu.
Kalliste imesema kuwa imefanikiwa kubadilisha seli za kawaida katika mbegu za kiume hadi mbegu za kiume zilizokomaa.
Category:
0 comments