CHAMA CHA DEMOCRATIC ALLIANCE CHATISHIA KUMNG'OA ZUMA MADARAKANI
Chama cha
Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya
kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa
uamuzi kuwa alikiuka katiba.
Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla.
Mamilioni ya madola yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na zizi la ngombe.
Category:
0 comments