MARUFUKU KUMILIKI LAINI MBILI ZA SIMU BURUNDI
Burundi imepiga marufuku umiliki wa laini mbili za simu kutoka kwa kampuni moja inayotoa huduma za mwasiliano ya simu.
Idhaa moja ya redio ya Bonesha FM imeripoti kuwa imepata taarifa hiyo kutoka kwa wizara ya fedha.
Kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano ya simu zimepewa kipindi cha miezi miwili kutekeleza sheria hiyo mpya.
Kampuni
hizo zitalazimika kusajili wamiliki wote wa laini za simu la sivyo
wataadhibiwa na faini ya takriban dola $3,000 kwa kila laini ambayo
itatumiwa pasi na kusajiliwa.
Sheria hii mpya imewekwa baada kutokea machafuko ya kisasa kwa takriban mwaka mooja sasa.
Machafuko nchini humo yalianza mwezi Aprili mwaka
uliopita baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula
wa tatu.
Wapinzani wake wanasema kuwa hatua hiyo ya Nkurunziza
inakiuka katiba ya taifa inayomzuia rais kuongoza kwa zaidi ya miaka 10
ama mihula miwili.
Nigeria iliiadhibu kampuni ya mawasiliano ya
MTN faini ya dola bilioni 5.2 kwa kuendelea kuruhusu utumizi wa simu
ambazo hazijasajiliwa.
Rais Muhammadu Buhari aliilaumu MTN kwa kuruhusu
wapiganaji wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi nchini humo kwa
kuruhusu laini za simu ambazo hazijasajiliwa kuendelea kutumika hata
baada ya ilani ya kutofanya hivyo.
Category:
0 comments