WATU 474 WAUWAWA BURUNDI
Takwimu mpya kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu 474 wamekwishauawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka jana, wakati mzozo ulipoibuka kufuatia uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu madarakani.
Wataalam watoa matokeo ya uchunguzi kutokana na ziara waliyoifanya nchini Burund mapema mwezi huu mbele ya Braza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini Geneva.Lakini kiongozi wa shirika la haki za binadamu la Burundi amesema kuwa idadi ya waliouawa inazidi watu 600.
Muakilishi wa serikali ya Burundia amesema kuwa mauji yalitekelezwa na waasi.
Jumanne, afisa wa ngazi ya juu wa kijeshi na mshirika wa rais alipigwa risasi na kuuawa kwenye ofisi ya wizara ya ulinzi.
Meja mwingine ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa usiku wa kuamkia leo alipokua akiondoka kwenye baa katikati mwa mji mkuu, Bujumbura.
Category:
0 comments