AC MILAN YAMTIMUA KAZI KOCHA WAKE
Asubuhi ya siku ya Jumanne imetoka taarifa kutoka katika klabu ya AC Milan kuhusu kufukuza kazi kocha wake, Sinisa Mihajlovic kufuatia kucheza michezo mitano bila kupata ushindi.
Kocha huyo wa zamani wa Sampdoria, Fiorentina na Serbia amefukuzwa kazi kufuatia kufungwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya wapinzani wao, Juventus kwa kipigo cha goli 2-1 na kusalia katika nafasi ya sita ya msimamo wa Ligi Kuu ya Italia (Seria A).
Baada ya kutimuliwa kazi, AC Milan imemteua kocha wa timu ya vijana wa klabu hiyo, Cristian Brocchi kuchukua nafasi ya Mihajlovic hadi msimu utakapomalizika.
Category:
0 comments