PROFFESA IVORY COST AFUNDISHA AKIWA AMEBEBA MTOTO MGONGONI
Profesa mmoja wa chuo kikuu amesifiwa pakubwa nchini Ivory Coast kwa kumbeba mtoto wa mmoja wa wanafunzi wake mgongoni wakati wa masomo.
Picha za Honore Kahi wa chuo cha Bouake, zimesambaa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Alisema aliamua kumsaidia mwanamke katika darasa lake wakati mtoto alipokua akilia wakati akiwa anaendelea na kipindi.
Picha zilizochukuliwa na mwanafunzi mwingine zinamuonyesha, bwana Kahi akifunza huku mtoto akiwa mgongoni tukio kama hili ni aghalabu sana kutokea katika nchi na karne ya sasa .
Category:
0 comments