WATU WAPATAO 80 WAFA KWA RADI
Maafisa nchini India wanasema kuwa watu 80 wameuwawa baada ya kupigwa na radi katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa taifa hilo katika muda wa saa 24 iliyopita.
Watu 53 walifariki katika jimbo la Bihar.Watu 10 waliuawa katika jimbo la mashariki la Jharkhand huku wengine 16 wakifariki katika eneo la Madhya Pradesh.Wengi waliuawa walipokuwa wakifanya kazi katika mashamba yao wakati huu wa msimu wa mvua.
Ni idadi kubwa sana ya watu kuuawa kwa mpigo mmoja ,jambo ambalo limewashangaza wengi.
Katika muongo uliopita, zaidi ya watu elfu mbili wamefariki kwa kupigwa na radi kote nchini India.
Ni vigumu sana kubashiri ni lini janga la radi litatokea na si rahisi kwa utawala kutoa tahadhari ya kutokea kwa radi.
Category:
0 comments