SYRIA AMANI YAPATIKANA LAKINI WANANCHI BADO HAWAAMINI KUHUSU KUDUMU KWAKE
![]() |
Syria |
Ni juma moja sasa tangu kusitishwa kwa mapigano ambayo yamepunguza sana uhasama nchini Syria. Kulikuwa na matukio machache ya mashambulizi hayo siku ya ijumaa Mashariki mwa mji mkuu wa Damascus.
Lakini katika maeneo mengine mashirika ya kutoa misaada yaliendelea na shughuli zake za kutoa huduma za kibinadamu, hata katika maeneo matatu yanayoshikiliwa na waasi na kuvamiwa mara kwa mara na wanajeshi wa Serikali.
hali ya utulivu katika maeneo hayo lakini raia wengi wa Syria hawaamini kuwa hali hiyo ya amani itadumu.

Mazungumzo ya amani kuhusu Syria Mashauriano ya awali ya amani yanatarajiwa kuanza tena mjini Geneva juma lijalo.
Hata hivyo kundi kubwa zaidi la waasi limeeleza wasiwasi wake kuwa huenda lisihudhurie mkutano huo.
Category: