CHANZO CHA NYIMBO YA HARMONIZE "BADO" CHAGUNDULIKA DIAMOND ALENGWA ZAIDI
Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema wazo la wimbo wake mpya ‘Bado’ aliyomshirikisha Diamond, lilikuja baada ya kumuuliza Diamond ni mwanamke gani ambaye ameachana nae lakini bado anashindwa kumsahau.
Akizungumza
katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Harmonize amesema baada
ya kupata wazo kutoka kwa Diamond ndipo akaanza kuandika wimbo.
“Idea
ilikuja kuna siku tulikuwa kwenye gari nikamuuliza (Diamond) kuna
mwanamke gani ulimpenda sana hadi leo unashindwa kumsahau, akaniambia
hakuna masihara kwenye mahusiano, mimi ndio nikapata idea,” alisema
Harmonize.
Aliongeza,
“Nikaona kama ni Diamond sio Diamond peke yake ambaye amekutwa na mambo
hayo kwenye mahusiano, hata mimi mwenyewe yameshanikuta. Kwa hiyo
nikaanza kuandika, nilivyoandika mistari yangu, nikampa producer akanipa
beat nikachagua. Baada ya hapo kwa sababu Diamond alikuwa Nigeria
alivyorudi siku nipo nae kwenye gari nikaiplay akaikubali akasema na
mimi nitaingiza verse ya pili,”
Tazama video hapa......
Tazama video hapa......
Category: