Kamishna wa Jumuiya ya Ulaya wa maswala ya wahamiaji amesema kuwa Ugiriki imefurika na wakimbizi na wahamiaji.
Dimitris
Avramopolous ametoa wito kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo ya Ulaya
kusaidia katika kusuluhisha hali hiyo badala ya kuiachia Ugiriki au
Italia pekee.
Kati ya wahamiaji 2003 wanakisiwa kuingia Ugiriki kila siku. Wengi wao hawawezi kusonga mbele kwa sababu ya vikwazo vikali vilivyowekwa na Austria na mataifa ya Balkan.
Wahamiaji wanaoingia Ugiriki
Mwandishi wa BBC anasema kuwa matamshi ya Bwana
Avromopolous ni ishara kuwa kiongozi huyo wa wahamiaji katika Jumuiya
hana nia ya taifa lake kuzuiliwa kuwa mwanachama wa muungano wa paspoti
wa Schengen.
Kwa kawaida mtu ye yote aliye na paspoti ya Schengen
ana uhuru wa kusafiri bila vikwazo kwa mataifa mengine wanachama wa
muungano huo.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.