MGOMBEA WA MAREKANI ACHEKWA MITANDAONI BAADA YA KUSHINDWA KUTAMKA TANZANIA IPASAVYO
Donald Trump achekwa mitandaoni baada ya kushindwa kutamka nchi ya Tanzania ipasavyo nakujikuta akijichanganya na kusema "Tan zay nia" kitu kilichosababisha kuleta gumzo katika mitandao ya kijamii kwa kiongozi mkubwa kama yeye kushindwa kuitamka nchi Maarufu na pekee duniani kwa uzalishaji wa madini ya Tanzanite.
Tukio hilo lilitokea wakati Bwana Donald Trump akiwa anaelezea sera yake ya kigeni na juu ya mashambulio ya kigaidi yaliotokea mnamo mwaka 1998 katika balozi za Marekani za nchini Tanzania huku gundi la kigaidi la Al Qaeda likihusishwa katika shambulio hilo
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli, yamkini jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari wa ikulu Bw Josh Earnest
Category:
0 comments