MMAREKANI AFUNGWA JELA MIAKA KUMI KOREA KASKAZINI KWA KOSALA UJASUSI
Picha juu raia wa Marekani Kim Dong-chul
Raia wa Marekani amefungwa jela kwa kipindi cha miaka kumi na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.
Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.
Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda.
Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.
Hata hvyo Korea kaskazini imeendelea kurusha makombora yake ya majaribio na kufanya umoja wa mataifa kuendelea kuinyooshea kidole nchi hiyo licha ya kuendelea kuiwekea vikwazo mbalimbali vya kiuchumi nchi hiyo
Category:
0 comments