AL SHABAAB WAUWA WANAJESHI 30

Wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, Al Shabab wanasema wamewauwa wanajeshi wa serikali zaidi ya 30.
Al Shabab, wanadai kutekeleza mauaji hayo walipoteka tena kijiji cha Runorgood, Kaskazini-Mashariki mwa mji mkuu wa Somali Mogadishu.Wenyeji wa kijiji hicho wamesema, kwamba kijiji chao kinadhibitiwa tena na wanamgambo wa Al Shabab.

Kwengineko nchini Somalia, watu kama watatu waliuwawa, kwenye shambulio la bomu, katika soko la mifugo huko Qoryoolay, inavoelekea shambulizi hilo lililengwa maafisa wa kukusanya kodi wa serikali.
Category:
0 comments