TANZANIA YA MAGUFULI WAFANYAKAZI WAPUNGUZIWA 2% YAKODI KATIKA MISHAHARA YAO

Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wanakila sababu ya kutabasamu.
Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi, bw Magufuli alitangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.
Hii inamaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.
Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu.
Aidha rais Magufuli alisema anatimiza ahadi aliotoa kwa wapiga kura wakati wa kampeini kuwa endapo watamchagua angefanya kila jitihada kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyikazi wa Tanzania.
Kuhusu ongezeko la mshahara wa chini zaidi atakaolipwa mtanzania bw Magufuli amewasihi wampe muda kidogo akomeshe rushwa na kuimarisha uchumi wa taifa kisha atatoa tangazo.

''aidha, amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.''
Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, ikulu Dodoma Gerson Msigwa ilisema.
Category:
0 comments