18 wapoteza maisha Mbeya
Watu wasiopungua 18 wameuawa katika ajali ya
gari mkoani Mbeya baada ya basi dogo la abiria kuanguka
na kutumbukia kwenye bonde lenye maji.
Mwandishi mmoja wa habari aliyefika eneo la
ajali ameeleza kuwa basi hilo dogo limetumbukia
bondeni katika eneo lenye mteremko mkali na
kona.
Polisi wanachunguza chanzo cha ajali, lakini
walioshuhudia wanadai dereva wa gari hilo
alikuwa akiwakimbia madereva wengine
waliotaka kumlazimisha aunge mkono mgomo wa
utoaji huduma unaoendelea kwa safari za kati ya
Mbeya na Kyela.
Imeelezwa kuwa madereva wa mabasi ambayo
kwa kawaida hutoa huduma kati ya eneo la Kyela
na Mbeya mjini walikuwa katika mgomo,
na kwamba hawakufurahishwa na basi hilo dogo
kuendelea kutoa huduma ndipo wakawa
wanamfukuza hatimaye akashindwa kulidhibiti
Ajali hiyo ni mwendelezo wa ajali mbaya za
barabarani kuhusisha magari ya abiria ambazo
zimetokea nchini kwa kipindi cha mwezi
mmoja uliopita.
Category:
0 comments