South Africa mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni
Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya
biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini
Afrika Kusini.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi
za mipira kutawanya umati kusini mwa mji wa
Johannesburg ambapo gari na nyumba
vilichomwa moto.
Msemaji wa polisi alisema kuwa karibu raia
mia mbili wa kigeni walikimbilia usalama kwenye
kituo cha polisi lakini wakaondoka muda
baadaye.
Maandamano ya kupinga uvamizi wa wageni
Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi
yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu
watano wameuawa.
Rais Jacob Zua amelaani ghasia hizo na
maandamano ya amani mjini Durban siku ya
Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu
kumi.
Category:
0 comments