Manchester united yaibuka kidedea.
Manchester United ilipanda tena katika nafasi ya
tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza ikiwa
pointi moja nyuma ya Arsenal baada ya
kuwacharaza mahasimu wao wa jadi Manchester
City mabao 4-2.
Sergio Aguerro alikuwa wa kwanza kuiweka City
kifua mbele lakini vijana wa Old Trafford
walisawazisha kupitia Ashley Young .
Kocha Pelegrini
Maruane Fellaini alifunga kichwa kizuri
kilichoiweka Manchester United kifua mbele kabla
ya kiungo wa kati Juan Mata kufunga bao zuri.
Chris Smalling alipiga kichwa kisafi
kilichomwacha kipa wa City bila jibu kabla ya
Aguero kufunga bao la kufutia machozi na la pili
kwa upande wa City ambo kwa sasa wamepoteza
mechi sita kati ya nane walizocheza.
Wachezaji wa manchester city
Katika mechi ya mapema viongozi wa ligi
Chelsea waliendelea na matokeo mazuri baada ya
kuwachapa wenyeji wao QPR bao 1-0.
Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas ndiye
aliyefunga bao hilo la pekee.
Category:
0 comments