.

.

Bi Hillary Clinton atangaza kugombea urais

ZePLAN | 00:49:00 | 0 comments

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa
Marekani, Bi Hillary Clinton ametangaza rasmi
kuingia katika kinyang'anyiro cha urais wa nchi
hiyo katika uchaguzi wa 2016 ambapo anataka
kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa
Marekani.
Alizindua ukurasa wake wa kampeni katika
mtandao wa internet, Jumapili, akiwaambia
Wamarekani kuwa anataka kuwa "kiongozi" wao.
Bibi Clinton aliingia katika mbio za kuomba
kuteuliwa na chama cha Democratic kuwa
mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008
lakini alishindwa kwa Bwana Barack Obama.
Akiwa mgombea anayepewa nafasi na
wanachama wa Democratic alitarajiwa kutangaza
azma yake ya kugombea miezi kadhaa iliyopita.
Katika video kupitia ukurasa wake wa kampeni,
Bibi Clinton alitangaza: "Nagombea urais".
"Wamarekani wamepambana na nyakati ngumu
za uchumi," amesema, "lakini hali imebaki
kuwanufaisha walio juu.
"Kila siku Wamarekani wanataka kiongozi na
nataka kuwa kiongozi," amesema
Bibi Clinton pia alikuwa mke wa rais wakati
mumewe Bill Clinton alipokuwa rais wa Marekan

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments