.

.

HOFU YA MABOMU YATAWALA NJOMBE TANZANIA

ZePLAN | 04:51:00 | 0 comments



Njombe. Wakazi wa Mji wa Njombe, jana walikumbwa na taharuki kutokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa na Polisi kwa lengo la kutawanya waandamanaji waliokuwa wanapinga mauaji ya mkazi mmoja anayedaiwa kupigwa risasi na askari na mwingine kujeruhiwa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Franco Kibona alisema jana kuwa hawezi kuzungumzia tuhuma hizo wakati hali ya kiusalama haijatulia.

Kamanda Kibona aliyekuwa eneo la tukio, aliwasihi wananchi kutulia kwani madai yao yanashughulikiwa.

Mauaji hayo yaliyotokea juzi usiku wakati wakazi hao wawili walipokuwa kwenye klabu ya pombe ya Nyondo, Mtaa wa Kambarage.

Wakazi wa eneo hilo walisema kuwa aliyeuawa ni Basil Ngole na majeruhi ni Fred Sanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe.

Wakazi hao walikusanyika hospitalini hapo saa moja asubuhi, huku wakipaza sauti za kulitaka Jeshi la Polisi kugharamia mazishi ya marehemu pamoja na matibabu ya majeruhi.

Kutokana na kadhia hiyo, polisi walifika eneo la tukio na kuwatawanya waandamanaji kwa mabomu na kusababisha mmoja ambaye ni dereva wa bodaboda kujeruhiwa.

Kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wananchi ambao waliziba barabara, kwa mawe, na kuchoma magurudumu ya gari

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments