AU YASUBIRI MAAMUZI YA BUNGE LA BURUNDI
Wabunge nchini Burundi wameanza
mjadala kuhusu hatua ya muungano ya Afrika wa kutuma kikosi cha
wanajeshi wapatao 5000 cha kulinda amani nchini humo, hatua ambayo
inafaa kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
AU hata hivyo imesema kuwa itasubiri hadi Jumanne kupokea majibu rasmi kutoka kwa serikali ya Burundi.
AU hata hivyo imetangaza kuwa itawapeleka majeshi ya kulinda amani nchini burundi iwe imekubali au imekataa.
Wabunge wanatarajiwa kupinga pendekezo la kutuma kikosi cha kudumisha amani nchini Burundi, kama ilivyopendekezwa na muungano wa Afrika.
Chama tawala cha CNDD_FDD kimesema kuwa mjadala huo usiokuwa wa kawaida utakaopeperushwa moja kwa moja kupitia kwa vyombo vya habari, ni wa kuwapa raia sauti kupitia kwa viongozi wao.
Kikosi hicho kitakuwa na kandarasi ya miezi sita ya mwanzo, na ambayo itaendelezwa.
Wanachama 54 wa muungano wa Africa walitangaza siku ya ijumaa kuwa watatuma kikosi cha wanajeshi 5000 kumaliza ghasia zinazoendelea, na ambazo zimeibua hofu ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Naibu msemaji wa rais Jean-Claude Karerwa amesema kuwa Burundi imeweka msimamo wake wazi, haitaki kamwe kikosi cha usalama kutoka nje nchini humo, na kuwa itachukua hatua iwapo kikosi hicho kitatumwa bila idhini ya serikali.
Ongezeko la ghasia nchini humo zimeibua hofu ya kutopkea kwa vita vya kiraia, mwongo mmoja baada ya vita vilivyodumu kati ya mwaka wa 1993-2006 kati ya waasi wa kabila la waHutu na majeshi ya watutsi, vilivyosababisha viofo vya watu laki 3
Category:
0 comments