POLISI ZAIDI YA 70 WAJERUHIWA VIBAYA UJERUMANI
Meya wa mji wa Leipzig nchini
Ujerumani ameeleza kushtuka kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wa polisi 70
waliokabiliana na waandamanaji waliokuwa wakipinga wafasisti hiyo jana.
Alisema kuwa vitendo vyao vilienda kinyume na kuhujumu yaliyopaswa kuwa maandamano ya amani ya kupinga makundi ya Kinazi mamboleo.
Waandamanaji wa mrengo wa kushoto walichoma mapipa ya uchafu na tairi na kutupa mawe, chupa na baruti za kujitengenezea katika juhudi za kuwazuia Wanazi mamboleo kuandamana.
Polisi kwa upande wao walitumia maji ya pilipili ya kutoa machozi .
Zaidi ya watu 20 walitiwa mbaroni.
Category:
0 comments