.

.

NYUMBA YA KIOGOZI WA MASHIA KASKAZINI MWA NIGERIA YAZINGIRWA NA WANAJESHI WA NCHI HIYO.

ZePLAN | 05:23:00 | 0 comments





Kundi moja la Waislamu Washia Kaskazini mwa Nigeria wanasema kuwa wanajeshi wamezingira makaazi ya kiongozi wao kufuatia mapigano ya jana ambapo watu kadhaa walifariki.
Kulingana na kundi la Islamic Movement of Nigeria, wanajeshi na vifaru vilitumika kushambulia makaazi ya Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria, jimbo la Kaduna.
Kundi hilo lilisema wafuasi wake watano waliuawa.
 
 
Wanajeshi na vifaru walitumika kushambulia makaazi ya Ibrahim Zakzaky mjini Zaria
Awali jeshi liliwalaumu mamia ya wafuasi wa kundi hilo la waislamu kwa kuzuia barabara moja na kufyatulia risasi msafara uliokuwa unambeba mkuu wa jeshi wa Nigeria.
Kundi hilo limakanusha madai hayo.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments