KISA CHA MSICHANA ANAETOA MACHOZI YA DAMU "MARNIE-RAE"
Huyu ni Marnie-Rae Harvey ambaye hutokwa na damu machoni lakini madaktari hawaelewi chanzo chake ni nini.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 anasema kuwa hawezi kutoka nje na hana marafiki kwa sababu kila mara huwa nyumbani kwao.Amewatembelea wataalam wa macho na madaktari wa maswala ya uzazi,madaktari wa watoto na wataalam wengine kujua sababu ya tatizo hilo.
''Inachoma na inapoziba jicho lango siwezi kuona'',aliimbia Newsbeat.
Hali hiyo isiyo ya kawaida pia huathiri masikio yake,pua,ufizi,kichwa,kucha na ulimi.
Hali hiyo ilianza baada ya kijana huyo kutoka eneo la Stoke-on-Trent kuanza kukohoa damu mnamo mwezi Machi 2013.
Hali hiyo iliendelea kwa kipindi cha miaka kadhaa hadi alipoamka usiku mnamo mwezi Julai mwaka 2015 akiwa uso wake umezibwa na damu.Alikuwa akitokwa na damu machoni.
Wazazi wake waliita ambyulensi ,madaktari waliofika walishangazwa sana na tukio hilo ambalo hawajaliona ,alielezea.
Nilipoenda hospitalini walinichunguza macho yangu lakini kila kitu kilikuwa sawa.
''Nilifanyiwa uchunguzi wa damu na matokeo yake yalikuwa sawa''.
Kwa kipindi cha wiki mbili zilizofuata macho yake yaliendelea kutokwa na damu.
Baadaye nilienda dukani na hapo macho yangu na masikio yalianza kuvuja damu ikalazimu ambyulansi iitwe tena.
Marnie-Rae alifanyiwa ukaguzi mwengine ,ambapo wataalam wengi walibaini kwamba ana kinga iliodhoofika.
Category:
0 comments