KOREA KASKAZINI KUINYOOSHEA KIDOLE MAREKANI, WATISHIA KUITWANGA MABOMU MAZOEZI YAENDELEA
Korea Kusini na Marekani hufanya mazoezi kila mwaka
Korea Kaskazini
imetishia kutekeleza mashambulio ya nyuklia dhidi ya Korea Kusini na
Marekani iwapo nchi hizo mbili zitaendelea na mazoezi ya pamoja ya
kijeshi.
Serikali ya Korea Kaskazini imetoa taarifa ya ikitishia kutekeleza “shambulio la nyuklia kwa ajili ya haki”.
Ni kawaida kwa Pyongyang kutoa vitisho vya aina hiyo na wataalamu wanatilia shaka uwezo wa Korea Kaskazini kuwa na makombora ya nyuklia.
Hisia hupanda kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini na Marekani kila mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi yanapofanyika.
Pyongyang hutazama mazoezi hayo kama mazoezi ya kujiandaa kuivamia.
- Korea Kaskazini kuweka tayari silaha za nyuklia
- Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini
- Korea Kaskazini yatangaza kamanda mpya wa jeshi
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imeionya Pyongyang dhidi ya “hatua za haraka zisizo za busara ambazo zinaweza zikailetea maangamizi”.
Yanaandaliwa siku chache tu baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini kutokana na hatua yake ya kufanyia majaribio bomu la nyuklia na kufyatua makombora.
Korea Kaskazini ilijibu vikwazo hivyo kwa kutangaza itaweka tayari silaha zake za nyuklia na pia ikavyatua makombora ya masafa mafupi baharini.
Category:
0 comments