KUMBE MNADA WA PUGU LILIKUWA JIPU ONA MAPATO YA SASA UKILINGANISHA NA KIPINDI KILICHOPITA
Habari za
kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato katika Taasisi nyingi za Serikali
zinazidi kuchukua vichwa vya habari, tuliona Jeshi la Polisi Usalama
Barabarani na sehemu nyingine mapato yakiongezeka. Leo Tarehe 11 March 2016 Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nao wameingia kwenye list ya ukusanyaji mapato mengi kwa kipindi kifupi.
Wizara hiyo imekusanya mapato ya mil 676.4 kuanzia December 19 2015 hadi March 9 2016, makusanyo haya yameongezeka baada ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nash
kuagiza Idara za Huduma za Mifugo na uzalishaji na masoko kufanya doria
ili kuhakikisha kwamba mifugo yote ambayo inanunuliwa kwenye minada ya
awali inapelekwa kwenye mnada wa upili uliopo Pugu Dar es salaam ili
kukaguliwa afya zao na kutolewa ushuru.
Ambapo
hapo awali wafanyabiashara walikuwa wakikwepa kupeleka mifugo yao ili
kukwepa ushuru wa Serikali, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara, Mkurugenzi wa Huduma za mifugo, Abdu Hayghaimo amesema..
Baada
ya kuanza kazi za doria na kudhibiti maeneo yote kuanzia machinjioni
hadi kwenye mnada wa pugu, mapato ya Serikali kwenye mnada wa pugu
yamepanda kwa wiki kutoka wastani wa sh mil 24 mwezi December 2015 kwa
wiki hadi sh mil 61 kwa wiki mwezi March 2016′
‘hii
inaonesha kwamba kabla ya doria kulikuwa na upotevu mwingi wa mapato ya
Serikali kwenye mnada wa Pugu na kwenye machinjio ya Mkoa wa Dar es
salaam‘
Category:
0 comments