MABAKI YA NDEGE INAYOSEMEKANA NI MALI YA NCHI YA MALYSIA YAPATIKANA MSUMBIJI NI BOEING 777
Malaysia imesema kuna uwezekano
mkubwa kuwa kifusi kilichogunduliwa Msumbiji cha ndege ya Boeing 777, ni
aina sawa na ile ya MH370
Waziri wa Usafiri wa Malaysia Liow Tiong Lai katika mtandao wake wa Twitter amesema timu yao ufundi inafanya kazi kwa kushirikiana na wenzao wa Australia kuweza kupata tena vifusi hivyo.
Ndege aina ya MH370 ilipotea mwaka 2014 wakati ikiwa safarini kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing, ikiwa imebeba abiria 239.
Licha ya msako wa kina uliofanywa chini ya maji, ulioongozwa na Australia ndege hiyo na abiria wake wote bado hawajapatikana.
Naye Waziri wa Miundombinuna usafiri wa Australia amesema vipande hivyo vilivyogunduliwa vitasafirishwa nchini mwake kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Kama itathibitishwa kama kiligunduliwa Msumbiji itakuwa ni kipande cha pili cha kifusi kutoka katika ndege kilichogunduliwa.
Kipande cha kwanza ambacho kilikuwa ni bawa la ndege kiligunduliwa katika ufukwe wa kisiwa cha Reunion.
Category: