WANAJESHI WA SUDAN KUSINI WALIUWA WATU ZAIDI YA SITINI
Shirika la haki za
binadamu la Amnesty International limelaumu wanajeshi wa serikali ya
Sudan Kusini kwa mauaji ya wavulana 60 pamoja na wanaume.
Amnesty International imesema vifo hivyo vilitokea nje ya kanisa katoliki katika mji wa leer Oktoba ya mwaka uliopita. Serikali ya Sudan imekanusha madai hayo.
Shirika hilo limeongeza walioshuhudia tukio hilo wamesema waliwasikia wafungwa hao wakilia na kupiga mayoe wakitaka kuondolewa kwenye bohari hilo.
Mashahidi hao waliambia Amnesty International kwamba waathiriwa hao walikua wafanyibiashara na wanafunzi na siyo wapiganaji.
Shirika moja la waangalizi wa vita Sudan Kusini limesema jeshi la serikali lilifahamu kuwepo kwa wafungwa hao ndani ya bohari hilo lakini walipuuza kuwaokoa.
Category:
0 comments