MAJIBIZANO MAKUBWA YAENDELEA BAINA YA KAMPUNI YA APPLE NA SERIKALI YA MAREKANI
Majibizano makali
yameendelea kati ya serikali ya Marekani na kampuni ya Teknolojia ya
Apple, baada ya kampuni hiyo kukataa kusaidia kufungua simu ya mmoja wa
washambuliaji waliowauawa watu kwa kuwapiga risasi mwezi Disemba.
Idara ya sheria iliwasilisha ombi mahakamani ikisema simu ya mshambuliaji huyo huenda ina ushahidi kuhusu shambulio hilo.
Pia idara hiyo imelaumu Apple kwa kuwa na ukaidi.
Kampuni
hiyo imejitetea na kusema shirika la ujasusi la FBI linatumia njia za
mkato ili kuweza kudukua simu zote kwa kutumia kisingizio cha simu moja.
Category:
0 comments