ALI KIBA AKUMBWA NA LAWAMA KUTOKA KWA MSANII MWENZAK
Msanii
Alikiba ametolea ufafanuzi tuhuma zilizotolewa na msanii mwenzake
Hakeem 5, huku akisema hataki hata kumuona kwani si mtu mzuri na
amekataa kufanya naye colabo.
Ali Kiba ameyasema hayo alipokuwa akiongea
kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na east africa Radio, na
kusema kwamba yeye binafsi hana tatizo na Hakeem 5, kwani yeye ni kama
ndugu yake, na hata deni lake la kolaboalishalipa, kwani alishafanya
naye kazi kabla hajachukua likizo ya kufanya muziki.
“Hakeem ni ndugu yangu na ataendelea kuwa ndugu katika dunia sikumtendea
mabaya, lakini hakuelewa vitu gani vinatakiwa viendelee sasa hivi, deni
ambalo anasema ananidai nililipa nikamfanyia nyimbo safi sana ndio
nikachukua ile likizo ya kufanya muziki kwa miaka mitatu, baada ya
likizo nikawa natangaza kurudi nikarudi vizuri, baada ya kurudi Hakeem
anataka tufanye video, mi nili-understand, lakini production ndio
tuliposhindwana”, alismea Ali Kiba.
Alikiba aliendela kuwa baada ya hapo kuna siku walikutana studio, na
Hakeem alimtaka tena Alikiba wafanye colabo, lakini Alikiba alishindwa
kufanya kolabo hiyo kutokana na mkataba aliokuwa nao kwa wakati huo
hakutakiwa kufanya kolabo yoyote, na ndipo alipochukia kwa kutoelewa.
“Nikakutana nae studio akawa anataka tufanye featuring, na kwa kipindi
hicho na mimi mkataba wangu sikutakiwa kufanya colabo, huwezi kuvunja
mkataba, sasa Hakeem hajanielewa”, alisema Alikiba
Category:
0 comments