APPLIKAKESHENI YA SIMU YA MTANDAO WA TALIBAN IMEONDOLEWA KWENYE SOKO LA GGOGLE
Alemarah, programu
inayotumiwa katika simu za Android iliyoundwa na kundi la wapiganaji wa
Taliban imeondolewa kwenye soko la programu la Google, Play Store.
Kundi hilo limesema kumetokea “hitilafu za kiufundi” baada ya app hiyo kutoweka.
Hata hivyo BBC imefahamu kwamba app hiyo imeondolewa kwa sababu inakiuka kanuni na sera za Google zinazokataa uchochezi.
App hiyo iligunduliwa na shirika la Marekani la Site Intel Group linalofuatilia shughuli za makundi ya kijihadi.
Google imekataa kuzungumzia app hiyo binafsi lakini ikasema kupitia taarifa kuwa: “Sera zetu zimeundwa kuridhisha wateja wetu na watu wanaotengeneza app. Ndio maana huwa twatoa apps zinazokiuka sera hizi kutoka kwenye Google Play."
Msemaji wa kundi la Taliban alikuwa ameambia Bloomberg kwamba app hiyo ilikuwa “sehemu ya juhudi za kiteknolojia za kufikia watu zaidi duniani.”
Category:
0 comments