KIONGOZI WA KUNDI LA KIGAIDI ATIWA NGUVUNI NCHINI NIGERIA
Jeshi la Nigeria limesema kuwa
limemkamata kiongozi wa kundi wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye
uhusiano pia na kundi la kigaigi la Al Qaeda.taarifa ya msemaji wa jeshi
la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid
al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo.
Ansaru ni kundi maarufu kwa utekaji wa raia kutoka nchi za Magharibi na limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia kadhaa wa kimagharibi pia.Brigedia Jenerali Rabe Abubakar amesema kuwa kukamatwa kwa Barnawi ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi.
“Ndiyo tumemkamata gaidi.Yeah, kukamatwa kwake ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi,na si ndani ya Nigeria tu bali duniani kote pia. Ni mtu mhimu sana katika makundi ya kigaidi Nigeria na Duniani,na tunajitahidi kuhakikisha hatuishii kumkamata yeye tu bali na wengine.
Category:
0 comments