MAANDISHI YA KIBAGUZI YAWEKWA UWANJANI NCHINI AUSTRALIA
Shirikisho la soka
nchini Australia limeshtumu mashabiki walioweka kitambara chenye
maandishi dhidi ya msikiti katika mechi moja huko mjini Melbourne siku
ya Ijumaa.
Maandishi hayo yalioonekana katika mechi kati ya
Collingwood na Richmond pia yalishirikisha nembo ya kundi la mrengo wa
kulia la United Patritic Front.
Hatahivyo kitambara hicho chenye maandishi kiliondolewa na mashabiki waliokiweka pia wakaondolewa uwanjani.
Shirikisho
la soka nchini humo mara kwa mara limekabiliwa na maswala ya ubaguzi
kufuatia kuzomwa kwa mchezaji mmoja wa Aborigine.
Mkuu wa
shirikisho hilo Gillon McLachlan amesema kuwa maandishi hayo yalikuwa na
ubaguzi,yaliwapuuza wengine na kuwakosea heshima.
Idadi ya waislamu nchini Australia ni asilimia 2.
Mnamo
mwezi Novemba ,utafiti ulionyesha kwamba waislamu wa Australia
wanakabiliwa mara tatu na ubaguzi unaokabili makabila mengine.
Category:
0 comments