RAIS MAGUFULI AFANYA UZINDUZI WA DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO NCHINI RWANDA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
Aprili 6, 2016 amezindua daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha
Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha
Rusumo. Zoezi hili la uzinduzi limefanyika kwa pamoja kwa husisha Rais Mhe. Dkt. Magufuli wa Tanzania na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, pia tukio hili limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Daraja
la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani ni kiungo
muhimu katika Ukanda wa Kati(Central Corridor), mtandao huu wa barabara
unaunganisha barabara kuu ya
Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro – Dodoma – Singida – Nzega – Tinde – Isaka – Lusahanga na Rusumo kupitia Kibingo Nakayonza hadi Kigali Nchini Rwanda. Mtandao huu utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli aliwahimiza Wananchi wa Nchi zote mbili kutumia fursa ya uwepo wa
Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani Rusumo kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Jumuiya yetu Afrika Mashariki kwa ujumla.

Aidha Mhe. Rais amewaasa Wananchi kulinda miundombinu kwani kuna baadhi ya wananchi wanadiriki kuiba alama za barabarani, vyuma vya madaraja na kuharibu taa za barabarani kwa baadhi ya miji, ameagiza vyombo vya usalama kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria kwa
wale watakaodiriki kufanya uharibifu huo.
Aidha licha ya mradi huo kurahisha usafairishaji wa bidhaa na watu Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa alieleza faida kadhaa za mradi huo zikiwemo; kuwa ni kiungo muhimu cha kuiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Kikanda kama vile SADC na COMESA, kurahisisha mawasiliano ya kijamii baina ya watu wa Tanzania na Rwanda, pamoja na kuimarisha uhusiano na kukuza biashara kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda na Nchi nyingine za Maziwa Makuu.
Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA.

Mradi
huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs.
33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa
kushirikiana
na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi – Mangaka.

wa Tanzania, Dk. Magufuli (katikati) akiwa pamoja na Rais wa Rwanda,
Paul Kagame na viongozi wa Serikali ya Tanzania na Rwanda pamoja na
wadau wa shirika wakiwa katika uzinduzi huo.
Category:
0 comments