Watu watano wakiwemo watoto watatu wa familia moja wamefariki wilayani Iramba,Mkoani Singida na wengine wawili kujeruhiwa kwa kuangukiwa na nyumba ya tembe wakati wakiwa usingizini kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia apr,sita mwaka huu na hatimaye nyumba yao ya tembe walikokuwa wamelala kuanguka na kuwakandamiza.

Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya ya Iramba ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama,Christopher Ngubiagai aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na Joseph Saidi,mkazi wa Kijiji cha Nguvumali,Mrisho Jumanne (4) mkazi wa Kijiji cha Misuna na watoto watatu wa familia moja kutoka Kijiji cha Nguvumali,kata ta Ndago.

“Ndugu waandishi ningependa kutoa taarifa fupi ya maafa yaliyotokea katika wilaya yetu ya Iramba,mimi kama kaimu mkuu wa wilaya ya Iramba jana(juzi) kuamkia leo (jana) kwa maana tarehe tano kuamkia tarehe sita usiku mvua zilinyesha katika wilaya zote mbili yaani wilaya za Iramba na Mkalama” alifafanua Ngubiagai.

Hata hivyo kaimu mkuu huyo wa wilaya ya Iramba aliweka bayana kwamba kutokana na mvua hizo kunyesha usiku,lakini mpaka sasa hakuna madhara yeyote yale yaliyojitokeza kwa wilaya ya Mkalama zaidi ya kutokea kwa vifo wilayani Iramba.

Aidha Ngubiagai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalma ya wilaya ya Iramba aliwataja pia waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Eliza Eliya (35) na Emmanueli Saidi (5) wote ni wakazi wa Kitongoji cha Ilongero,Kijiji cha Nguvumali,kata ya Ndago,wilayani hapa.

Kuhusu vifo vya watoto hao wa familia moja,Ngubiagai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya za Mkalama na Iramba aliweka wazi kuwa watoto hao walitumbikia kwenye dimbwi lililojaa maji wakati walipotoka nje kwenda kujisaidia baada ya mvua kuancha kunyesha.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,ambaye pia ni Ofisa kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya hiyo,Mariether Kasongo alisema baada ya ajali iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku, Halmashauri inaendelea kufanya tathimini ya uharibifu uliotokana na mvua hiyo.
“Kabla ya maafa tuliwataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na taarifa tulizopatiwa na idara ya hali ya hewa za kupatikana kwa mvua katika kipindi hiki cha mwezi,kwani taarifa tulizonazo ni kwamba mvua zinaweza kunyesha zaidi ya wastani au chini ya wastani”alisisitiza kaimu mkurugenzi huyo.

Kutokana na taarifa hizo za hali ya hewa,Kasongo alisema ndipo walipochukua tahadhari kwa kuwajulisha wananchi, maafisa watendaji wa kata na vijiji wanaoishi mabondeni na kwenye maeneo yenye mafuriko waanze kujiandaa kukabiliana na mvua hizo za masika.

Hata hivyo hakusita kuwasisitiza juu ya kuzitumia mvua hizo kwa kulima mazao ya mizizi kama vile viazi vitamu,mihogo pamoja na dengu kutokana na mazo hayo kukomaa kwa muda mfupi 

DSCN0005Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wakiwa katika moja ya vikao vyake vya kutoa mauzia kisheria sambamba na shughuli za maendeleo

DSCN0031Mbunge wa jimbo la Iramba mashariki,(Mkalama),Bwana Allani Kiula(wa kwanza kutoka kushoto) akiwa katika moja ya mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama na kushoto kwake ni katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Bi Ernestina

DSCN5003Mkuu wa wilaya ya Mkalama ambaye kwa sasa pia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Iramba,Mkoani Singida,Bwana Christopher Ngubiagai akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwangeza,wilayani Mkalama