SINGIDA NA KILIO CHA MADAWATI KATIKA WILAYA YA MKALAMA MKUU WA WILAYA APATA JAWABU
WILAYA
ya Mkalama mkoani Singida,inatarajia kufanya harambee kubwa aprili tisa
mwaka huu, kwa lengo la kukusanya shilingi 150 milioni zitakazotumika
kununulia madawati 2,500 kwa matumizi ya shule za msingi na sekondari.
Harambee
hiyo ya aina yake,itasimamiwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher
Ngubiagai na inatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Nduguti makao makuu
ya wilaya hiyo.
Ngubiagai
alisema wamefikia uamuzi huo wa kufanya harambee,ikiwa ni sehemu ya
kutekeleza agizo la rais Dk.Magufuli kuwa ifikapo juni 30,kila shule ya
msingi na sekondari nchini,iwe imejitosheleza kwa madawati.
Aidha,
alisema utekelezaji wa agizo hilo ni kuunga mkono ahadi ya elimu bure
iliyotolewa na rais wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika
oktoba mwaka jana.
“Niliporipoti
kuanza kazi wilaya ya Mkalama oktoba mwaka jana,wilaya yetu ilikuwa na
upungufu wa madawati 6,773.
Tumehamasisha vya kutosha na nashukru wadau
mbalimbali wameweza kutuchangia madawati 478 na sasa tuna upungufu wa
madawati 6,295 ambayo gharama yake ni shilingi 377,7 milioni “,alisema.
Mkuu
huyo wa wilaya,alisema kwenye harambee,wanatarajia kukusanya shilingi
150 milioni na kiasi kingine kitatoka kwenye mfuko wa mbunge pamoja na
benki ya NMB iliyoonyesha nia ya kusaidia kumaliza tatizo la madawati.
“Natoa
wito kwa wadau wote wa sekta ya elimu,wazawa wa wilaya hii walioko
ndani na nje ya wilaya na taasisi mbalimbali wahudhurie harambee hiyo
bila kukosa.Lengo letu ni kwamba tuimbe wimbo moja nao ni kumaliza
‘upungufu wa madawati’ katika wilaya yetu”amesisitiza.
Katika
hatua nyingine,Ngumbiagai alitumia fursa hiyo kumpongeza mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Mkalama,kwa juhudi zake za kuhamasisha
watumishi wa chini yake kushiriki kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi
wa madawati.
“Dead
line ya rais Magufuli juu ya upungufu wa madawati,haipo mbali,hivyo
tunapaswa wakazi wa wilaya ya Mkalama tuunganishe nguvu zetu,ili kila
shule ya msingi na sekondari,iwe na madawati ya kutosha na ikiwa na
madawati ya ziada,itapendeza zaidi”,amesisitiza zaidi Dc Ngubiagai.
Category:
0 comments