ALIKIBA APATA SHAVU SOUTH AFRIKA
Nyota wa mziki wa kizazi kipya Alikiba yupo nchini Afrika kusini katika mji wa Johannesburg akiwa katika safari zake za kikazi .
Baada tu ya kufika Johannesburg Alikiba alialikwa na shabiki wake kwenye duka maarufu la kuuza vifaa vya muziki Afrika Kusini linalomilikiwa na raia wa South Africa nakumpa nafasi ya ya kuchukua bure kitu chochote kwenye duka hilo lililo sheheni vifaa mbalimbali vya mziki ,hii inatokana na mapenzi tuu kutoka kwa shabiki huyo juu ya msanii Alikiba .
Hata hivyo kwenye safari hiyo Alikiba ameambatana na waandishi na wanahabari mbalimbali na wakati wote mpaka anapewa mualiko walikuwa wameambatana pamoja kutoka kwenye hilo duka akiwa ameambatana na Meneja wake Seven na Watangazaji Millard Ayo na B12 wa CloudsFM.
Category:
0 comments