.

.

KOREA KUSINI,JAPAN NA MAREKANI WAJIFUA KIJESHI KUPAMBANA NA MAKOMBORA

ZePLAN | 01:47:00 | 0 comments

wanajeshi wa Japan                

Korea Kusini, Marekani na Japan zimefanya zoezi la ushirikiano la kukabiliana na makombora katika maji ya jimbo la Hawaii.
Hatua hiyo inajiri kufuatia msururu wa majiribio ya makombora ya masafa mafupi katika miezi ya hivi karibuni inayofanywa na Korea kaskazini.
                                                  
Majaribio mengi hatahivyo hayakufanikiwa lakini ufanisi wa kombora la sita hivi majuzi ulilishangaza eneo hilo.
Korea Kaskazini ambayo imefanya majaribio manne ya mokombora ya kinyuklia imesema kuwa zoezi hilo ni la uchokozi wa kijeshi.
                   Zoezi la kijeshi                
Vyombo vya habari vimesema kuwa Marekani pamoja na vikosi vyengine ni tishio la mara kwa mara la usalama wa Korea Kaskazini na hivyo basi kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na makombora ya masafa marefu na yale ya kinyuklia.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments