ALIECHUKUWA TUZO YA DIAMOND HUYU HAPA NI DJ NA PRODUCER MAARUFU AFRIKA KUSINI
DJ raia wa Afrika Kusini ambaye pia ni producer maarufu kama Black Coffee, ameanikiwa kuibuka kidedea mble ya wanamuziki maarufu wakiwemo WizKid, Yemi Alade na Diamond Platnumz na kushinda tuzo ya BET nchini Marekani.
Mwaka uliopita Black Coffee alitoa albamu yake ya tano, Pieces of Me, na kupata mashabiki wengi.
Mwaka 2015 na 2016 umaarufu wake uling'aa katika ulingo wa kimataifa maeneo tofauti kote duniani.
Hata hvyo msanii wa Tanzania Nasib Abdul (Diamond Platinum) ameendelea na ziara zake kama alivyokuwa amezipanga awali huku mashabiki wake lukuki wa ndani na nje ya Afrika mashariki wakimpa moyo na kumpongeza kwa hatua kubwa ya kimziki aliyofikia na kuwa msanii wa kwanza kuiwakilisha Tanzania katika tasnia ya mziki kwenye tuzo hizo za BET Award.
Category:
0 comments