SCOTLAND YASUBIRIA KUFANYA UAMUZI JUU YA KUJITENGA NA UMOJA WA ULAYA
Kuna uwezekano mkubwa wa Scotland kupiga kura upya ya kujitenga na Uingereza.
Kiongozi mkuu wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema kwamba kufuatia kura ya kujiondoa kwa muungano wa EU, sasa ni bayana kuwa hatma ya baadaye ya watu wa nchi yake wanajiona kuwa sehemu ya EU.
Matamshi ya Sturgeon yanafuatia matokeo yaliyodhihirisha kuwa kila eneo wakilishi la Scotland lilipiga kura kusalia kwenye muungano wa Ulaya EU wala sio kujiondoa.
Waandishi habari wanasema kuwa, uwezekano wa kuwepo kwa kura nyingine ya maoni ya iwapo Scotland isalie kuwa sehemu ya Uingereza au la umeongezeka mara dufu.
Mwenyekiti wa chama cha Irish Republican, Sinn Fein, maarufu kama (Declan Kearney), amesema kwamba kura ya Uingereza imechochea kesi ya kuitisha kura ya maoni kuhusiana na umoja wa Ireland.
Mbunge wa chama pinzani cha Labour, Keith Vaz, ameitisha wito wa kufanyika kwa kongamano la dharura kwa mataifa ya EU; huku akisema matokeo ya kura hiyo ni jambo la kutisha kwa Uingereza.
Hata kabla matokeo hajakuwa bayana, wafuasi wa chama cha Conservative wa mrengo uliotaka Uingereza iondoke, wametia saini taarifa ya gazeti moja inayomtaka waziri mkuu David Cameron kusalia ili kurekebisha kura hiyo ya maoni.
Naye kiongozi mkuu wa chama chama UK Independence, Nigel Farage, amemuomba Bwana Cameron kujiuzulu.
Category:
0 comments