CHINA YAINYOOSHEA MAREKANI KIDOLE
Kuizuia China katika kisiwa ilichojenga katika maji yanayogombaniwa huenda kukasababisha mvutano mkubwa, chombo cha habari cha serikali ya China kimsema.
Majibu hayo ya hasira yanajiri baada ya waziri mteule wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kusema kuwa Marekani inapaswa kuizuia Beijing kuingia katika visiwa vipya katika bahari ya kusini mwa China.Magazeti mawili yalikashifu matamshi hayo .
Jarida la Global Times limeonya kwamba hatua kama hiyo inaweza kusababisha vita vikubwa.
Beijing imekuwa ikitengeneza visiwa katika miamba ya maji yanayogombaniwa na mataifa mengine.
Picha zilizochapishwa mwaka uliopita zinaonyesha ulinzi mkali katika baadhi ya visiwa hivyo.
Akizungumza siku ya Jumatano Bwana Tillerson aliifananisha visiwa hivyo vya China na hatua ya Urusi kuchukua eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine.
''Tutalazimika kuieleza China kusitisha ujenzi wowote katika visiwa hivyo na kwamba kuingia katika visiwa hivyo pia hakutaruhusiwa''.
Msemaji wa Wizara ya maswala ya kigeni ya China Lu Kang amenukuliwa akisema: China ina haki kutekeleza vitendo vyovyote katika himaya yake.
Na ilipouliwa kuhusu matamshi ya kuizuia China ,alijibu: siwezi kujibu maswali yasio na msingi.
Category:
0 comments