NIGERIA :CHUO KIKUU CHASHAMBULIWA NA MABOMU
Raia wawili na walipuaji wawili wa kujitoa kufa, wamefariki katika shambulio la bomu kwenye Chuo Kimoja kikuu nchini Nigeria.
Milipuko hiyo miwili ya kujitoa mhanga iligonga Chuo Kikuu cha Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Yamkini watu wanne wameuwawa, wakiwemo walipuaji hao wa kujitolea kufa.
Msemaji
wa polisi amesema kuwa, walimkabili mmoja wa washambuliaji
hao - msichana wa umri wa miaka 12 hivi, katika lango la Chuo hicho.
Huku akishukiwa kubeba bomu, walimpiga risasi, na hapo ndipo bomu alilokuwa amejifunga likalipuka.
Watu 15 wameripotiwa kujeruhiwa
Kwa muda mrefu mbinu za kutumia milipuko ya mabomu ya kujitoa mhanga yamekuwa yakitumika na kundi la Boko Haram, mara nyingi wakiwatumia wasichana wadogo.
Huku serikali ya Nigeria ikidai kuwafurusha wanamgambo wa Boko Haram kutoka katika makao yao waliokuwa wakiyadhibiti, inaonekana kuwa wapiganaji hao wa kiislamu wangali bado wanaweza kushambulia.
Kumekuwepo ongezeko la mashambulio ya aina hii, inayopenya hadi mmji mkuu wa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Category:
0 comments