NDEGE YA ABIRIA YAPONEA CHUPU CHUPU KUGONGANA NA NDEGE ISIO NA RUBANI MJINI LONDON
Ndege moja ya abiria ilinusurika kugongana na ndege isiyokuwa na rubani umbali wa futi 10,000, wakati ilikaribia kutua uwanja wa Hethrow mjini London.
Marubani walikiona kifaa kilicho ni sehemu kadha wakati ndege ikiwa inakaribia kutua.
Maafisa katika uwanja wa ndege walisema kuwa marubani walishangaa kuona kifaa hicho kikiruka umbalia kama huo na kusababisha taharuki .
Ndege hiyo isiyo na rubani ilikadiriwa kuwa umbali wa mita 30 kutoka ndege ya abiria.
Ndege kubwa zisizo na rubani hazistahili kupaa umbali wa futi 400 angani au karibu na viwanja vya ndege.
Polisi walijulishwa kuhusu kisa hicho lakini hawakumpata mwenye alikuwa akielekeza kifaa hicho.
Ndicho kisa cha hivi punde cha ndege ya abiria kukaribiana sana na ndege isiyo na rubani na kufikisha visa kama hivyo kuwa 59 ndani ya miezi 12.
Category:
0 comments