Kiongozi wa islamic brotherhood ahukumiwa kunyongwa
Mahakama moja nchini Misri imethibitisha
hukumu ya kifo ya kiongozi wa kundi la Muslim
Brotherhood Mohammed Badie na watu wengine
13 kwa kupanga mashambulizi dhidi ya serikali.
Pia mahakama hiyo imemfunga maisha raia
mmoja mwenye uraia wa Marekani na Misri na
watu wengine 36.
Badie alipewa hukumu hiyo mnamo mwezi Machi
na pia anakabiliwa na mashtaka mengine.
Hatahivyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu
hiyo.
Mamia ya watu wamehukumiwa kifo katika
msako dhidi ya wanachama wa kundi hilo
kufuatia kuondolewa kwa rais Mohammed Morsi
mwaka 2013.
Hatahivyo ,kufikia sasa ni mtu mmoja pekee
aliyenyongwa.
Uamuzi huo wa mahakama ulitangazwa moja
kwa moja na runinga za taifa hilo.
Hukumu hizo ni za mwisho katika kesi ambayo
viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood
walishtakiwa kwa kuwachochea wanachama wa
kundi hilo kuanzisha ghasia dhidi ya serikali
kufuatia maandamano ya mwaka 2013.
Mshirikishe mwenzako
Category:
0 comments