.

.

Kenya yatoa tamko UN

ZePLAN | 13:14:00 | 0 comments

Serikali ya Kenya imeupatia Umoja wa Mataifa
makataa ya miezi mitatu kuwahamisha
wakimbizi wa Somalia wapatao nusu milioni
hadi nchini Somalia.
Naibu rais William Ruto amesema kuwa iwapo
Umoja wa mataifa utakataa kuwahamisha
wakimbizi hao, Kenya itachukua jukumu la
kuwandoa.
Makataa hayo yanajiri siku kadhaa baada ya
shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo
takriban watu 148 waliuawa na kundi la
wapiganaji wa Al-shaabab.
Wakimbizi Dadaab
Baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakiishi katika
kambi za Dadaab mashariki ya taifa hilo kwa
zaidi ya miongo miwili.
Kenya imelishtumu kundi la Alshabaab kwa
kujificha katika kambi hizo huku likiwasajili
wanachama wapya.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments