.

.

Kocha wa Man City Pellegrin asema kuhusu mgogoro kwenye club yake

ZePLAN | 13:24:00 | 0 comments

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester City Manuel
Pellegrini amesisitiza kuwa kilabu yake haiko
katika mgogoro .
Raia huyo wa Chile anatapatapa kukoa kazi yake
kama mkufunzi huku timu hiyo ikipambana na
Manchester United siku ya jumapili katika mechi
ya debi itakayochezwa uwanjani Old Trafford.
Manchester City imeshuka hadi nafasi ya nne
kufuatia msururu mbaya wa matokeo baada ya
kushinda mara mbili pekee kati ya mechi saba.
Pellegrini
Kocha Pellegrini amewaona wapinzani wake
Arsenal na Manchester United wakipanda katika
jedwali katika majuma ya hivi karibuni na sasa
anajua kwamba atasalia kuwa mkufunzi wa
kilabu hiyo iwapo atafanikiwa kuiweka timu hiyo
katika nne bora zitakazofuzu katika mashindano
ya kuwania kilabu bingwa Ulaya msimu ujao.
Wachezaji wa Mancity
Baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo tayari
wameanza kuhusishwa na uhamisho katika timu
nyengine huku Pellegrini pia akiwa hajui iwapo
atanedelea kufunza timu hiyo msimu ujao.
Na sasa anakabiliwa na kibarua kigumu cha
kukabiliana na mahasimu wao wa jadi siku ya
jumapili ambao wameshinda mechi zao za
mwisho sita .

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments