SAUDI ARABIA:Marubani wakivita wapewa zawadi baada ya shambulizi
Mwana wa mfalme nchini Saudi Arabia ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini humo, ameshambuliwa katika mitandao ya kijamii baada ya kuwapa magari ya kifahari marubani wa ndege za kivita wa nchi yake ambao walishiriki katika kampeni ya kurusha mabomu na kuishambulia Yemen.
Mwanzoni mwa wiki hii Saudi Arabia iliweka bayana mwisho wa awamu ya kwanza ya kampeni yake ya kijeshi nchini Yemen.Katika sherehe za kufurahia matokeo ya kampeni hiyo ya kwanza mwana wa mfalme Al-Waleed bin Talal, ,aliweka maoni yake kwenye ukurasa wake wa twitter wenye wafuasi milioni tatu akisema kwamba; kwa kutambua na kuonesha nimethamini kile walichofanya askari wetu kwenye awamu hii ya kwanza ,ninajisikia fahari kuwazawadia askari ambao ni marubani pia wapatao mia moja magari aina ya Bentley kwa matokeo mazuri ya oparesheni yetu .Pendekezo la zawadi hiyo kutoka kwa mawana wa mfalme lilikumbwa na upinzani mkali mara tu baada ya kuwekwa katika mtandao huo wa kijamii na kuwagawa wafuasi wake katika makundi mawili, zaidi ya wafuasi wake elfu ishirini na nane walitumiana ujumbe huo na zaidi ya wafuasi wake elfu tano waliupenda ujumbe huo.
Mwana wa mfalme huyo alisifiwa kwa moyo wake wa ukarimu na wasaudia wengi, ambao walitoa maoni yao juu ya uamuzi wake huo,na kusema kwamba marubani hao wanastahili magari hayo ya kifahari na zaidi ya hayo kwa kazi yao nzuri ya kutukuka waliyoifanya nchini Yemen.
Hata hivyo ujumbe huo wenye kutoa zawadi nono kwa marubani hao umefutwa katika akaunti yake ya twitter,ingawa hapo awali ujumbe huo ulishasambazwa na unaendelea kusambaa mitandaoni.
Na baadhi ya vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vimeripotiwa kudai kuwa akaunti ya mwana wa mfalme ilikuwa imedukuliwa ,ingawa hakukuwa na taarifa yoyote hapo awali iliyolalamikia udukuzi huo ,na mwana wa mfalme huyo mpaka sasa ameamua kupiga kimya, wala hajasema neno.
Mwaka uliopita, mwana mfalme huyo,anayetambuliwa kwa mahaba yake ya kupenda maisha ya kifahari na mwenye mkono mwepesi wa kutoa zawadi kubwa kubwa ,mwaka huo inaarifiwa kuwa aliipatia timu ya mpira wa miguu ya nchi hiyo magari ishirini na matano baada ya kushinda michuano ya kandanda ya nchi hiyo,suala ambalo lilizua mjadala yakwamba nani anapaswa kutoa zawadi nchini humo na nani hastahili kutoa zawadi.
Category:
0 comments